Mwanamuziki kutoka Uganda Ronald Alimpa amekanusha tuhuma za wizi wa wimbo wa wa kabaka Atumye zilizoibuliwa na msanii mwenzake Baby J.
Katika mahojiano yake hivi Alimpa amesema ameshangaza na hatua ya Baby J kudai kuwa aliiba ubunifu wa wimbo wake wa Kabaka Atumye na kuutumia kwenye wimbo wake mpya bila ridhaa yake.
Hitmaker huyo wa Seen Don amesema aliandikiwa wimbo huo na uongozi wake hivyo hakujua kama kuna wimbo wa Baby J ambao una jina sawa na wake.
Msanii huyo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba yuko tayari kukutana na Baby J kwa ajili ya kutatua tofauti zao.
Utakumbuka mwaka wa 2017 Baby J aliachia wimbo uitwao kabaka Atumye chini ya Climax Records lakini wimbo huo haukupokelewa vyema na wapenzi wa muziki mzuri nchini Uganda kama ilivyo kwa tolea la Ronald Alimpa.