You are currently viewing RONALD ALIMPA AKANUSHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYAA

RONALD ALIMPA AKANUSHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYAA

Mwanamuziki kutoka Uganda Ronald Alimpa amekanusha madai yanayosambaa mtandaoni kuwa mraibu wa dawa za kulevya.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Alimpa amesema tuhuma hizo hazina ukweli wowote kwa kuwa hatumii kabisa mihadarati katika maisha yake.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Seen Don” amesema madai hayo yameibuliwa na watu wenye nia ya kumpaka tope huku akikiri mara ya mwisho kutumia bangi ilikuwa mwaka wa 2016 lakini kilichomkuta kilimfanya achane na matumizi ya dawa hizo.

Kauli ya Ronald Alimpa imekuja mara baada ya promata mmoja nchini Uganda kudai msanii huyo alimdhalilisha kwa kumpulizia moshi ya bangi usoni walipomteka nyara pamoja na timu yake kufuatia mzozo uliobuka kati yao aliposusia kutumbuiza kwenye shoo yake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke