You are currently viewing RONALDO AKANUSHA MADAI YA UONGO DHIDI YAKE YALIYOIBULIWA PASCHAL FERRE

RONALDO AKANUSHA MADAI YA UONGO DHIDI YAKE YALIYOIBULIWA PASCHAL FERRE

Nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo amesema Mhariri wa Kandanda nchini Ufaransa Paschal Ferre aliongea uongo, pale aliposema matumaini pekee ya Ronaldo ni kuhakikisha anastaafu akiwa na tuzo za Ballon d’Or nyingi zaidi ya Lionel Messi.

Paschal Ferre ambaye ni Mratibu wa tuzo za Ballon d’Or aliyasema maneno hayo wakati akizungumza na kituo kimoja cha habari nchini Marekani, ambapo alisema Ronaldo alimwambia atahakikisha anastaafu akiwa na Ballon d’Or zaidi ya Messi.

“Siku zote nashinda kwa sababu yangu na wale wanaonipenda, sishindani na mtu”, aliandika Ronaldo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Ronaldo ameongeza kuwa hajawai hata siku moja kuongea maneno ya kusema anataka tuzo nyingi, hata hivyo amesema Ferre alitumia maneno kama hayo kutengeneza na kusafisha jina lake pamoja na kutengeneza “tension” ya tukio jambo ambalo ameliita kuwa siyo sahihi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke