Cristiano Ronaldo kurejea ndani ya Manchester United kumesababisha mshambuliaji wa timu hiyo, Bruno Fernandes kupoteza ubora wake.
Hayo ni maoni ya nguli wa timu hiyo, Andy Cole ambaye ameeleza kuwa Wareno hao wanapata shida kucheza pamoja.
Fernandes alikuwa staa wa timu na kuonyesha ubora wa juu lakini ameshindwa kuwa katika ubora wa juu msimu huu.
“Kila kitu kimebadilika, Bruno hajawa yule alivyokuwa, ni kama ana hofu ya Ronaldo, nafikiri hatakiwi kuwa na hofu kwa kuwa wote ni wachezaji wakubwa,” alisema Cole.