You are currently viewing ROSA REE AFUNGA NDOA YA SIRI NA MPENZI WAKE WA MUDA MREFU

ROSA REE AFUNGA NDOA YA SIRI NA MPENZI WAKE WA MUDA MREFU

Female rapper kutoka nchini Tanzania Rosa Ree amethibitisha kufunga ndoa ya kimya kimya na mpenzi wake wa muda mrefu alie mtambulisha kama King Petrousse huko Moshi, Kilimanjaro..

Rosa Ree ametumia ukurasa wake wa Instagram kushare mfululizo wa picha zenye ujumbe unaoashiria kuwa sasa ameingia rasmi kwenye ndoa akiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni yanayovaliwa kwenye ndoa za Kinyarwanda, ‘Umushanana.

Picha hizo za Rosa Ree na mpenzi wake Petrouse imeibua hisia za mashabiki wake na mastaa wenzake ambao wameenda mbali na kumpongeza msanii huyo kwa hatua hiyo kubwa maishani.

Ikumbukwe Rapper huyo na mchumba wake wa tangia wakisoma shule ya sekondari, king petrousse wamekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa kipindi cha miaka mitano na waliweka wazi mahusiano yao kwa umma mwezi Septemba mwaka huu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke