Msanii wa Bongofleva, Rosa Ree amefuta picha zote za mchumba wake, King Petrousse katika ukurasa wake wa Instagram.
Hatua hiyo inakuja mara baada ya miezi hivi karibuni Rosa Ree kutokuonekana kuposti sana picha za King Petrousse kama ilivyokuwa hapo awali.
King Petrousse alimvisha Rose Ree pete ya uchumba Septemba mwaka jana, kisha kwenda Zanzibar kwa ajili ya mapunziko.
Utakumbuka baada ya hatua hiyo, King Petrousse alioneka kwenye video ya wimbo wa Rosa Ree, Mulla akimshirikisha Abby Chams iliyotoka Desemba 2022.