Rapa wa kike kutoka Tanzania Rosa Ree ametangaza rasmi ujio wa album yake mpya iitwayo “Goddess” ambayo ameitaja kuiandaa kwa takribani miaka minne.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amebainisha kwamba, anaachia album yake hiyo kama msanii anayejitegemea mwenyewe yani adhaminiwi na lebo yoyote na wala hajauza muziki wake kwa kampuni yoyote ya usambazaji wa muziki.
Hitmaker huyo wa “Watatubu” amesema kampuni nyingi zilimfuata kutaka kumdhamini lakini amesema amechagua kumiliki muziki wake kwa asilimia mia.
Hata hivyo ameeleza kuwa albamu yake hiyo itaingia sokoni Novemba 26 mwaka huu, huku akisema album ya Goddess ina aina mbalimbali za muziki ambazo zinamtambulisha yeye ni nani hasa.