You are currently viewing ROSE MUHANDO AKANUSHA TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA LORD MUTAI

ROSE MUHANDO AKANUSHA TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA LORD MUTAI

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili kutoka nchini Tanzania Rose Muhando amejitenga na tuhuma za kutoka kimapenzi na mwanablogu mwenye utata nchini Lord Mutai.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Rose Muhando amekanusha madai hayo kwa kusema kwamba hayana msingi wowote ikizingatiwa kuwa hamfahamu kabisa Lord Mutai.

Kauli Rose Muhando imekuja mara baada ya mtumiaji mmoja wa mtandao wa Twitter kwa jina la Bookten kudai kuwa hitmaker huyo wa ngoma ya  “Nibebe” aliwahi kutoka kimapenzi na mwanablogu maarufu wa Twitter nchini Kenya Lord Mutai huko mjini Thika kwenye moja ya Hoteli aliyokuwa akifanya kazi.

Bookten alienda mbali zaidi na kusema kwamba alimfumania Lord Mutai akimsindikiza Rose Muhando hadi kwenye chumba kimoja cha hoteli hiyo ambapo walilala hadi asubuhi.

Hata hivyo baada ya taarifa hiyo kuzua gumzo mitandaoni Lord Mutai aliibuka na kujitenga na madai hayo kwa kusema kuwa hajawahi kutoka kimapenzi  na Rose Muhando katika hoteli yoyote mjini Thika ambapo alienda mbali zaidi na kutishia kumfungulia mashtaka Bookten kwa hatua ya kumpaka tope.

 

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke