You are currently viewing ROSE MUHANDO ATUHUMIWA KUTOKA KIMAPENZI NA MWANABLOGU MAARUFU NCHINI KENYA LORD MUTAI

ROSE MUHANDO ATUHUMIWA KUTOKA KIMAPENZI NA MWANABLOGU MAARUFU NCHINI KENYA LORD MUTAI

Msanii mashuhuri wa nyimbo za injili nchini Tanzania rose Muhando ameusimamisha mtandao wa Twitter kwa Jina lake kukaa kwenye orodha ya ‘Topics’ ambazo zinazungumzwa zaidi kwenye mtandao huo nchini Kenya.

Hii ni baada ya mtumiaji mmoja wa mtandao wa Twitter kwa jina la bookten kudai hitmaker huyo wa ngoma ya  “Nibebe” aliwahi kutoka kimapenzi na mwanablogu maarufu wa Twitter Lord Mutai.

Kulingana na Bookten aliwahi kufanya kazi kama mpokea wageni katika eneo la burudani liitwalo Club Image mjini Thika na alimuona Lord mutai akimsindikiza rose muhando hadi kwenye chumba cha hoteli katika klabu hiyo.

Booktena alienda mbali zaidi na kudai kuwa bwana mutai alilala na rose muhando kwenye chumba hicho hadi asubuhi akihoji kuwa walishiriki tendo la ndoa.

Hata hivyo bwana mutai amejitenga na madai hayo akisema kuwa hajawahi kutoka kimapenzi  na rose Muhando katika hoteli yoyote mjini Thika. Mutai amesema mawakili wake kwa sasa wako kwenye harakati ya kufuatilia shutuma zilizoibuliwa dhidi yake na Bookten.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke