Msanii wa muziki Bongofleva, Rosa Ree amefunguka kuhusu kusainiwa kwenye lebo ya Rick Ross, Maybach Music Group.
Akizungumza na XXL ya Clouds FM, Rosa Ree amesema anafurahia kuona Rick Ross kakubali muziki wake na mambo yatakapokuwa tayari mashabiki wake tafahamu.
“Kiukweli nashukuru kuona Rick Ross mtu ambaye nimekuwa nikimsikiliza tangia nipo shule anakuwa anakubali kitu ambacho nakifanya, hata nilipotoa wimbo wangu wa mwisho, Blueprint alitoa maoni kwamba ni kitu kizuri”.
“Mambo ni mazuri kwa sababu tunawasiliana, tunaongea na huwezi kujua yajayo yanaweza kuwa ni makubwa sana, sitaki kufichua chochote napenda mfahamu ni kitu gani kitakuwepo huko mbele pindi tutakapokuwa tayari” alisema Rosa Ree.
Ikumbukwe toka ameanza muziki Rosa Ree amepita kwenye lebo kama The Industry na Dimo Production ya Afrika Kusini.