Mwanamuziki mwenye asili ya Nigeria Rotimi amefichua sababu kwa nini anataka kuwa na watoto wengi.
Akizungumza kwenye video iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa Instagram Juzi, Rotimi alikiri kwamba kuwa mtoto wa pekee katika familia yao kulimfanya kutaka kuwa na watoto wengi.
“Kwa hiyo nataka mwanangu (Seven Adeoluwa Akinosho) awe na mtu ambaye anaweza kumtegemea, ambaye anamuangalia. Wanajua watakuwa pale kwa ajili yake. Binti yangu akiangalia upande wake wa kulia, anajua ana kaka mkubwa ambaye anapitia jambo lile lile katika umri huo huo.” alisema Rotimi na kuongeza kuwa hakutaka kusubiri muda mrefu sana kupata watoto.
“Unajua sikutaka lile pengo la miaka sita, saba ambapo kimsingi ni watoto tu, kwa hiyo nilitaka wawe karibu sana kiumri na Vanessa alielewa na yeye alitaka jambo hilo hilo. Nilihisi kuwa na mwenza huyo.” alieleza Rotimi. Mapema mwezi huu wawili hao walitangaza kuwa wanataraji