Mgombea wa wadhfa wa useneta kaunti ya Nairobi msanii Rufftone amezua gumzo mtandaoni mara baada kuibuia madai mazito dhidi ya kaka yake Daddy Owen.
Akiwa kwenye moja ya interview Rufftone amesema miaka kadhaa iliyopita Daddy Owen ambaye kwa wakati huo alikuwa mfuasi sugu wa Chama ODM alimkimbiza kwa panga nusra amkatekate na tangia kipindi hicho hajawahi kipenda chama hicho kwani anakihusisha na uhuni.
Hitmaker huyo wa “Mungu Baba” alishindwa kueleza kwa kina mfumo wa uchumi wa bottom up ambao unaendesha na chama cha UDA ambacho kinaongozwa na Naibu wa rais Dkt William Ruto.
Hata hivyo ametoa wito kwa wakenya kuwachagua viongozi vijana ambao watabadilisha taifa hili kwa kuleta maendeleo mashinani.