Hitmaker wa “Girlfriend”, Msanii Ruger amemkataa hadharani Stevo Simple Boy baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kama ana wimbo wa pamoja na msanii huyo wa Men In Business.
Ruger ambaye yupo nchini kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki amesema hamjui kabisa msanii huyo huku akithibitisha ujio wa ngoma yake na kundi la Sauti Sol ambayo itapatikana kwenye album yake mpya mwakani.
Utakumbuka juzi kati Eric Omondi alithibitisha ujio wa kolabo ya Stevo Simple Boy pamoja na msanii huyo kutoka nchini Nigeria mara tu atakapotua nchini.
“At this rate wacha sisi tutengeneze Pesa watu ni Viziwi hawaskii maneno. The only Event happening in Mombasa this December. 28th December Wild waters. Na Stivo Somple boy ashajishindia Collabo na Ruger. GET YOUR TICKETS from my BIO @sofire_53 @sofire_fiesta”, Aliandika Instagram
Ruger anatarajiwa kutoa burudani leo kwenye tamasha la So Fire Fiesta litakalofanyika Nyali, Mombasa.