Mwimbaji wa nyimbo za injili aliyegeukia ukasisi Ruth Matete amewaonya wanawake dhidi ya kutongoza wanaume.
Kwenye mahojiano na Lupaso TV, Matete amesema kitendo hicho kinakwenda kinyume na maandiko matakatifu lakini pia ni kuidhalilisha jinsia ya kike.
Kulingana na mama huyo wa mtoto mmoja, wanaume ndio wanapaswa kuwa wa kwanza kuwatokea au kuwatongoza wanawake na sio vinginevyo.
Mwimbaji huyo amewashauri wanawake kumgeukia Mungu kwenye suala la kumtafuta mume mwema atakayekidhi matamanio yao badala ya kwenda kinyume na itakidi za kijamii.
Hata hivyo amefichua kuwa yupo single na anatafuta mwanaume wa ndoto yake ambaye anamzidi kiumri kwani ni watu ambao wana malengo kwenye maisha.
Utakumbuka Ruth Matete alijipata kwenye njia panda baada ya kumpoteza mume wake John Apewajoye kwenye ajali ya moto mwaka 2020.
Hata hivyo baada ya mume wake kufariki watu walimshambulia mitandaoni wakidai huenda alihusika moja kwa moja kwenye kifo cha mume wake huyo madai ambayo aliyekana.