You are currently viewing RUTH MATETE AWEKA WAZI MATAMANIO YAKE YA KUINGIA KWENYE NDOA

RUTH MATETE AWEKA WAZI MATAMANIO YAKE YA KUINGIA KWENYE NDOA

Msaniii Ruth Matete amefunguka kuhusu suala la kuingia kwenye mahusiano mengine.

Kupitia Instagram mama huyo wa mtoto mmoja amesema hivi karibuni atafikisha umri wa miaka 40 na anatamani kupata watoto zaidi ya wawili kabla hajafunguka ukurasa wa kuzaa.

Mshindi huyo Tusker Project fame amesema kwa sasa yupo mbioni kumtafuta mwanaume wa ndoto yake ili waweze kufunga pingu ya maisha.

Kutokana na changamoto ya kumtafuta mchumba Ruth matete amesema huenda akatumia njia za kitabibu kupata watoto mapacha na njia hiyo isipofanya kazi atamtafuta mwanaume ambaye yupo tayari kumsaidia kufanikisha ndoto yake hiyo.

Utakumbuka Ruth Matete alijipata kwenye njia panda baada ya kumpoteza mume wake John Apewajoye kwenye ajali ya moto

Hata hivyo baada mume wake kufariki watu walimshambulia mitandaoni wakidai huenda alihusika moja kwa moja kwenye kifo cha mume wake huyo madai ambayo aliyekana.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke