You are currently viewing SAILORS GANG WATANGAZA UJIO MPYA

SAILORS GANG WATANGAZA UJIO MPYA

Kundi la muziki wa Gengetone Sailors Gang limetangaza kurejea rasmi kwenye game ya muziki nchini baada ya ukimya wa miaka miwili.

Wasanii wanaounda kundi hilo wamethibitisha taarifa hiyo kwenye mahojiano yao ya hivi karibuni huku wakiwataka mashabiki zao wakae mkao wa kula kupokea ujio wao mpya ambao wameutaja ni wa kitofauti sana ikizingatiwa kuwa wana mpango wa kuachia ngoma mfululizo bila kupoa.

Wasanii hao wamekanusha tetesi za kuacha muziki kama inavyoripotiwa mitandaoni ila walichukua mapumziko mafupi kwa ajili ya kujipanga vizuri kimuziki.

Ikumbukwe kundi la Sailors Gang ambalo linaundwa na wasaani Miracle Baby,Masilver na Shalkido lilijipatia umaarufu mwaka wa 2019 kupitia muziki wa gengetone ambao unapendwa na vijana wengi nchini.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke