Sakata la ndoa ya msanii KRG The Don na mkewe Linah wanjiru linaendelea kuwaka moto.
Mtandao wa Nairobi gossip umeripoti kwamba, Linah Wanjiru ameorodhesha kiasi ambacho anataka alipwe na KRG The Don baada ya kuachana.
Linah amesema anahitaji kiasi cha shillingi elfu 350 za kenya kwa mwezi kwa ajili ya matunzo yaani Spousal Support.
Linah ambaye amezaa motto mmoja na KRG The Don, anayatolea macho mamilioni ya pesa ya msanii huyo wa muziki ambapo pia amemtaka amlipie ada ya mawakili wake kwa ajili ya mchakato mzima wa kufungua shauri la talaka miezi michache iliyopita.