You are currently viewing SAKATA LA NDOA YA MSANII LEVIXONE NA DESIRE LUZINDA LACHUKUA SURA MPYA

SAKATA LA NDOA YA MSANII LEVIXONE NA DESIRE LUZINDA LACHUKUA SURA MPYA

Msanii aliyegeuki muziki wa Injili nchini Uganda Desire Luzinda inadaiwa kuwa hajafunga ndoa na mwimbaji mwenzake Levixone kwa nia njema kwani anamtumia kwa ajili ya kupata msaada wa kifedha kutoka kwa wafadhili.

Chanzo cha karibu na mrembo huyo kinasema kipindi Desire anaanzisha wakfu wake Desire Luzinda Foundation alijaribu kuomba msaada kwa kanisa ambalo anashiriki nchini Marekani lakini alikataliwa kwa sababu hakuwa ameolewa.

Uongozi wa kanisa hilo ulimshauri kuingia kwenye ndoa kwanza kama mkristo kamali ili aweze kupewa msaada wa kufadhili wakfu wake.

Sasa rafiki yake wa zamani mwimbaji Levixone ndiye alikuwa kimbilio kwake na inatajwa hiyo ndio sababu ya mrembo huyo kuficha mahusiano yake ya kimapenzi.

Hata hivyo wawili hao hawajatoa tamko lolote dhidi ya tuhuma hizo ila ni jambo la kusubiriwa.

Utakumbuka video ya Levixone akiwa anatambulishwa kwa wazazi wa Desire Luzinda ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kitendo ambacho kiliwaacha walimwengu na maswali  juu ya wawili hao kuhalalisha mahusiano yao.

Hii ilikuja mara baada ya uvumi wa wawili hao kutoka kimapenzi kuzungumziwa sana mtandaoni kwa kipindi cha miezi miwili.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke