You are currently viewing SAKATA LA STEVE NYERERE NA SHIRIKISHO LA WANAMUZIKI TANZANIA LACHUKUA SURA

SAKATA LA STEVE NYERERE NA SHIRIKISHO LA WANAMUZIKI TANZANIA LACHUKUA SURA

Msanii wa Bongofeva Nay wa Mitego ameunga mkono kauli ya Mwana FA kutoa saa 48 kwa Shirikisho la Muziki Tanzania kuanza upya mchakato wa kumtafuta msemaji mpya kwa mujibu wa vigezo vilivyopo.

Machi 21 wasanii mbalimbali wa muziki walikutana katika kikao jijini Dar es Salaam kujadili sakata hilo, huku wengi wakisema Steven Nyerere hawezi kuwa msemaji wala mhamasishaji wa muziki.

“Kauli ya Mwana FA watu wasiichukulie kama kauli ya kibabe, kitemi na kutumia nafasi yake kama Mbunge lakini haya ni mawazo ya wasanii wengi ambao hawana nafasi ya kuongea na woga wakiamini Steve ni mtu wa ndani na ana-connection. wengi hatuungi mkono maamuzi ya shirikisho, na hiyo ni kauli yetu sio ya Mwana FA”

“Kama mtu hana sifa za uongozi tukikubali atuongoze ni kama tumekubali bora yaende. yasiwe masaa 48, yawe hata masaa 24. Steve tunakupenda kama msanii wa kuchekesha lakini sio msemaji na afisa mipango wetu” amesema Nay.

Hata hivyo, hapo awali Steve Nyerere alisema hana mpango wa kujiuzulu kama msemaji wa Shirikisho la wanamuziki Tanzania muda mchache tu baada ya wasanii hao kumpa saa 48 kufanya hivyo.

“Nimeshateuliwa na kuchukua majukumu yangu kama Msemaji na Mratibu wa mipango ya shughuli za muziki na katu siwezi kung’atuka hata kwa dawa. Nawaambia tu, sijiuzulu na wala sitoki, Nina nia ya kuendeleza sanaa ya nchi hii,” amesema Steve Nyerere.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke