You are currently viewing Samuel Eto’o aomba radhi kwa kumshambulia Mwandishi wa Habari

Samuel Eto’o aomba radhi kwa kumshambulia Mwandishi wa Habari

Rais wa Shirikisho la Soka nchini Cameroon, Samuel Eto’o ameomba radhi kufuatia kitendo chake cha kumpiga na kumshambulia kwa mateke Mwandishi wa Habari mnamo Disemba 5 mwaka huu.

Kwenye video ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya Kijamii, Eto’o alionekana akimshambulia Mwandishi huyo ambaye ni raia wa Algeria. “Ningependa kuomba radhi kwa kushindwa kuzuia hasira zangu na kufanya kitendo ambacho hakiendani na utashi wangu.” ameandika Eto’o.

Kwenye msamaha huo ambao ameutoa hadharani, Mshambuliaji huyo wa zamani wa Cameroon alitueleza kisa cha kwanini alifikia uamuzi huo wa hasira na kumpiga Kijana huyo. Amesema ni chuki na maneno ya dhihaka ambayo yanaendelea toka kwa mashabiki na Wananchi wa Algeria kufuatia kuondolewa na Cameroon kwenye kuwania tiketi ya ushiriki wa Kombe la Dunia 2022.

Tangu ushindi wa mabao (2-1) na Cameroon kupita kwa sheria ya bao la Ugenini March 29 mwaka Jana, vita, uhasama na chuki vimekuwa vikimuandama Samuel Eto’o toka kwa mashabiki wa Algeria wakidai kwamba Cameroon ali-cheat pasina ushahidi wowote. Aidha ameliomba Shirikisho la Soka nchini Algeria pamoja na mamlaka husika kukomesha hili kabla ya majanga makubwa hayajatokea.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke