Msanii kike nchini Sanaipei Tande amezua gumzo mtandaoni mara baada ya kudai kuwa mapromota na madeejay wa Kenya wamekuwa wakimtaka kimapenzi kabla ya kumpa nafasi ya kutumbuiza kwenye matamasha ya muziki.
Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamemtaka sanaipei tande aweke wazi majina ya mapromota na madeejay hao wanaoendeleza kadhia hiyo ili wasanii wachanga waweze kuwaepuka.
Utakumbuka wiki kadhaa zilizopita Sanaipe Tande alikiri hadharani kuwa kuna mmoja wa wanahabari tajika nchini alimtaka kimapenzi ili ampe michongo itakayobadilisha maisha yake.