Staa wa muziki nchini Sanaipei Tande ameteuliwa kushiriki kwenye tuzo za Women in Film Awards (WIFA) kwa mwaka wa 2021.
Sanaipei ametajwa kuwania kipengele cha TV Drama akichuana na waigizaji kama Ann Stella Karimi, Jacky Matubia,Mercy Mueni, Ann Stella Karimi na Michelle Chebet Tiren.
Tayari zoezi la kupiga kura kwa ajili ya kuwachagua washindi wa vipengele mbali mbali linaendelea hadi Februari 15 mwaka wa 2022 kupitia mitandao ya kijamii ya Women In Film Awards.
Tuzo hizo ambazo zinafanyika kwa mara ya nne nchini Kenya zilianzishwa kwa lengo la kutambua mchango wa wanawake katika tasnia ya filamu ambayo inazidi kukua kwa kasi katika siku za hivi karibuni.