Kundi la muziki nchini Sauti Sol limetangaza kuja na tamasha spesheli kwa mashabiki wao wa kigeni ambao hawatapata nafasi yà kuhudhuria show yao ya Sol Fest wikiendi hii.
Kupitia ukurasa wao rasmi wa Instagram Sauti Sol wamesema Desemba 13 mwaka huu wataanda tamasha spesheli kwa mashabiki zao walioko nje ya Kenya kwa ushirikiano na umoja wa ulaya kenya.
Wakali hao wa Ngoma ya “Suzzana” wamesema tamasha hilo litaruka mubashara kupitia channeli yao ya mtandao wa Youtube kuanzia saa kumi alasiri ambapo wametaka mashabiki zao kukaa mkao wa kula kwa show hiyo ambayo itakuwa moto wa kuotea mbali.
Ikumbukwe Desemba 12 mwaka huu Sauti Sol wanatarajiwa kutumbuiza jijini Nairobi kwenye tamasha lao la muziki la Sol Fest ambalo wamekuwa wakiipiga upata kwenye mitandao ya kijamii