Kundi la Sauti sol limeingia ubia wa kufanya kazi na jukwaa la Shahara lilowapa fursa watengeneza maudhui kutangaza kazi zao za ubunifu kwa njia ya mtandao.
Sauti sol wamethibitisha taarifa hiyo njema kwa mashabiki wao kupitia ukurasa wao wa Instagram kwa kushare picha wakiwa wanatia saini mkataba wa maelewano na Shahara huku wakieleza furaha yao ya kujiunga na familia ya Shahara ambayo imekuja na mpango wa kuwasaidia watengeneza maudhui kunufaika na kazi zao za sanaa.
Wakali wa ngoma ya “Suzzana” wamesema Shahara itawapa nafasi wanaounda mahudhui kumiliki kazi zao za ubunifu sambamba na kuwafungulia njia ya kuwafikia watu wengi zadi huku wakipata kipato kupitia maudhui wanayopakia kwenye mtandao huo tofauti na majukwaa mengine.
Kwa sasa Sauti Sol watatakiwa kutangaza huduma za Shahara kwa mashabiki zake ambao ni wabunifu kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuiongeza jukwaa hilo idadi kubwa ya watengeneza maudhui watakaochapisha kazi zao kwa njia ya mtandao.