You are currently viewing SAUTI SOL WAPINGA UTEUZI WA DKT. EZEKIEL MUTUA KUWA MWENYEKITI WA MAMLAKA INAYOSIMAMIA HAKIMILIKI NCHINI KENYA

SAUTI SOL WAPINGA UTEUZI WA DKT. EZEKIEL MUTUA KUWA MWENYEKITI WA MAMLAKA INAYOSIMAMIA HAKIMILIKI NCHINI KENYA

Wasanii wa Sauti Sol, Bien Baraza na Chimano kwa kauli moja wamepinga uteuzi wa Dakta Ezekiel Mutua kama mwenyekiti wa Mamlaka inayosimamia  Hakimiliki nchini Kenya.

Kupitia jumbe walizochapisha kwenye mtandao wa Instagram wasanii hao wameonekana kutofurahisha na kitendo cha Mutua kupewa wadhfa huo huku wakisema kuwa hawana imani na uongozi wake ikizingatiwa kuwa alishinda kuiboresha sekta ya filamu kipindi anahudumu kama mwenyekiti wa Bodi ya filamu.

Kauli yao imekuja mara baada ya dakta Ezekiel mutua kusema kwamba anafuraha kurejea kwenye sekta ya muziki kama mwenyekiti wa Mamlaka inayosimamia hakimiliki nchini ambapo aliahidi kuwapigania wasanii wa Kenya hadi pale muziki wao utakapowaingiza kipato kwani  muziki ni ajira kwa vijana kwenye mataifa yaliondelea.

Utakumbuka Daktari Mutua alihudumu kama afisa mkuu mtendaji katika bodi ya filamu nchini (KFCB) kati ya mwaka 2015 na 2021, ambapo alichukiwa na wengine kwa kujaribu kulainisha kazi za sanaa na maadili nchini.

Muda wake katika bodi hiyo ulifikia kikomo mwezi Agosti mwaka 2021 baada ya tume ya kupambana na ufisadi nchini kuanzisha uchunguzi dhidi yake na mmoja wa wanachama wa bodi ya filamu kwa kupokea marupurupu na mishahara kwa njia isiyofaa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke