You are currently viewing SAUTI SOL WAPOKEA CHETI CHA UTAMBUZI KUTOKA GRAMMY

SAUTI SOL WAPOKEA CHETI CHA UTAMBUZI KUTOKA GRAMMY

Kundi maarufu la muziki nchini, Sauti sol limepokea cheti cha utambuzi yaani (Certificate of Recognition) kutoka kwa waandaji wa tuzo za Grammy.
 
Cheti hicho ni maalum kwa ajili ya ushiriki wao kama watayarishaji kwenye album ya msanii Burna Boy kutoka Nigeria iitwayo “Twice As Tall” ambayo ilishinda tuzo ya Best Global Music Album kwenye tuzo za 63 za Grammy zilizofanyika mwezi wa tatu mwaka huu.
 
Sauti sol wameshiriki kwenye uandaaji wa wimbo namba 11 kutoka kwenye album ya “Twice As Tall” uitwao ‘Time Flies’.
 
Ikumbukwe, Sauti Sol kwa sasa wapo nchini Uingereza kwa ajili ya ziara yao ya kimuziki baada ya mapumziko ya takribani miaka miwili kutokana na janga la Corona.
 
 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke