You are currently viewing Sauti Sol watoa tamko baada ya tamasha la Sol Fest kupata ukosoaji mkubwa mtandaoni

Sauti Sol watoa tamko baada ya tamasha la Sol Fest kupata ukosoaji mkubwa mtandaoni

Kundi  la Sauti Sol limetoa tamko baada ya mashabiki kujitokeza kwenye mitandao ya kijamii na Kuwatupia lawama juu ya kuchelewa kupanda jukwaani kwenye Tamasha la Sol Festival lililofanyika wikiendi hii iliyopita nchini Kenya.

Mashabiki walidai kuwa walikaa muda mwingi kuwasubiria mastaa hao licha ya kuwa tamasha lilikuwa ni lao lakini walifika Alfajiri na kutumbuiza kwa muda mchache kisha kuondoka jukwaani.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram sautisol, waliwashukuru mashabiki kwa kufanikisha tamasha hilo huku wakiahidi kufanya makubwa kwenye hafla ijayo ya Sol Fest.

“Tunapenda kuwashukuru na kuwahakikishia mashabiki wetu wote kwamba tutajipanga vyema wakati mwingine na tuwaalika kutoa maoni ya kuboresha tamasha letu lijalo,” sehemu ya ujumbe wao umesomeka.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki hawakuridhika na taarifa hiyo huku wakihoji ni kwa nini hawajaomba radhi kwa kitendo chao cha kufika jukwaani kwa kuchelewa.

“Msamaha uko wapi?” aliuliza mtumiaji mmoja wa Instagram.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke