You are currently viewing Sauti Sol waweka wazi pesa wanazotoza makampuni kutumia nyimbo zao kwa matangazo

Sauti Sol waweka wazi pesa wanazotoza makampuni kutumia nyimbo zao kwa matangazo

Wasanii wa kundi la Sauti sol wameweka wazi kiasi cha pesa wanacholipishwa kwa makampuni ambayo yanalenga kutumia nyimbo zao kwenye shughuli za kibiashara.

Kwenye mahojiano na Ayo TV wasanii hao wakiongozwa na Bien Aime Baraza amesema wanatoza shillingi millioni 12 kwa matangazo huku akibainisha kuwa hawalipishi mashabiki wanaotumia nyimbo zao kwa ajili ya kujiburudisha.

Lakini pia wamezungumzia umuhimu wa wasanii wa Afrika Mashariki kuwa na umoja kwenye suala kuupeleka muziki wa ukanda huu kimataifa kwa kuwataka washirikiana kwenye nyimbo zao kama njia moja ya kubadilisha mashabiki.

Hata hivyo wamedokeza ujio wao mpya kama kundi kwa kuwataka mashabiki wakae mkao wa kupokea kazi zao mpya ikizingatiwa kuwa wana mpango wa kuachia album mpya mwakani (2023).

Utakumbuka mara ya mwisho wasanii wa sauti sol kufanya kazi pamoja ilikuwa mwaka 2020 kupitia Album yao ya Midnight Train.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke