Kundi la Sauti Sol limezindua rasmi jukwaa la watoto liitwalo Sol Kids Kenya, ambalo linalenga kuja na vitabu vya watoto vitakavyowaelimisha kuhusu haki zao, kujilinda na ujuzi wa kujieleza.
Kupitia ukurasa wao wa Instagram Sauti Sol wamesema jukwaa hilo la mtandaoni litatoa mchango mkubwa katika kuboresha elimu miongoni mwa watoto kwa kutoa vitabu vya vya hadithi na mashairi vitakavyowasaidia kujenga kumbukumbu, uelewa, na kupata ujuzi wa kutatua matatizo.
Wakali hao wa ngoma ya Suzzana wamesema wameamua kuja na wazo la Sol kids kutokana na kukosekana kwa jukwaa maalumu linaloshughulikia vitabu vya watoto jambo ambalo limepelekea baadhi ya watoto kumaliza shule bila ya kuwa na uwezo wa kusoma na kuandika.
Mbali na hayo member wa sauti sol, Fancy Fingers maarufu kama Polycarp Otieno alipata fursa ya kuzindua kitabu chake cha pili kiitwacho lala land baada ya written in the stars ya mwaka wa 2021 ambayo ni mahsusi kwa ajili ya watoto kujifunza ili kuongeza maarifa.
Kitabu chicho cha hadithi kinapatikana kwenye majukwaa kadhaa ya kuuza vitabu mtandaoni ikiwemo App ya Sauti Sol iitwayo Hustle sasa kwa shillingi 999 za Kenya.