Zoezi la ugawaji wa tuzo za muziki za AFRIMMA kwa mwaka 2021 limehitimishwa usiku wa kuamkia huko Multiple Venues nchini Marekani.
Mastaa kadhaa wameweza kujishindia tuzo hiyo kubwa ya muziki kama vile Wizkid, Flavour, Fally Ipupa, Focalistic,Ruger na wengine wengi, pia tumeshuhudia tena wasanii kutoka Tanzania na Kenya wakiendelea kufanya vyema.
Mwaka huu Afrika mashariki tumewakilisha vyema na ushindi kutoka kwa Diamond Platnumz aliyeshinda tuzo ya Msanii Bora wa kiume Afrika Mashariki, Nandy akishinda tuzo ya Msanii Bora wa kike Afrika Mashariki na kundi la Sauti Sol ambao wameshinda tuzo ya kundi bora Afrika Mashariki.
Hata hivyo, Msanii pekee aliyepata Tuzo nyingi ni Wizkid kutoka Nigeria, kupitia wimbo wake wa Essence ambapo ameshinda jumla ya Tuzo 2 za Afrimma 2021 ikiwemo tuzo ya Msanii bora wa mwaka na msanii aliye vuka mipaka nje ya mipaka yaani ‘Crossing Boundaries With Music Awards’