You are currently viewing SAVARA ADAI HAAMINI KWENYE SUALA LA WANANDOA KUVISHANA PETE

SAVARA ADAI HAAMINI KWENYE SUALA LA WANANDOA KUVISHANA PETE

Msanii Savara ametoa ya moyoni kwa kusema kwamba haamini kwenye suala la wapenzi kuvishana pete wanapofunga ndoa.

Msanii huyo wa Sauti Sol amehoji kuwa pete haina umuhimu wowote kwa wanandoa, hivyo haoni kama inaashiria uaminifu kwa kuwa ni pambo kama mapambo mengine.

Kwenye mahojiano na podcast ya SPM Buzz Savara amesema kuna watu wamevishwa pete na wapenzi wao lakini mwisho wa siku wanafanya udanganyifu kwenye mahusiano yao.

Hata hivyo amesisitiza kuwa penzi la kweli linatoka moyoni na wala sio kupitia pete, hivyo hatokuja kumvisha pete mchumba wake Yvonne Endo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke