Mwimbaji wa Sauti Sol Savara Mudigi ametia nia ya kufanya kazi ya pamoja na rapa Meek Mill.
Kauli yake imekuja mara baada ya rapa huyo kutoka nchini Marekani kutoa tangazo kupitia ukurasa wa twitter kwamba anamtafuta msanii kutoka Afrika ambaye atamshirikisha kwenye album yake mpya.
Utakumbuka mapema mwaka huu akiwa nchini Ghana Meek Mill aliweka wazi mpango wa kumsaini msanii kutoka Afrika kwenye lebo yake, Dream Chasers Records.