Msanii wa Sauti Sol, Savara ametangazwa kuwa balozi mpya wa knywaji cha Kenya Cane
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Savara amesema ni jambo la faraja kufanya kazi na Kenya Cane kwani huo ni mwanzo wa ushirikiano mzuri kati yake na kampuni hiyo.
Lakini pia ameishukuru uongozi wake pamoja na wadau wote waliofanikisha dili hilo huku akiahidi kuiongezea kampuni hiyo mauzo kutokana na ushawishi kwenye jamii.
“I have worked hard to bring out my genius through art. I am on my journey to more greatness and I am proud to partner with Kenya Cane as the Official Brand Ambassador.
I appreciate all parties that made this possible. I love my team. Now to more amazing art. Twende kazi #TheGreatsToastTwice”, Ameandika Instagram
Hata hivyo Kampuni ya Kenya Cane imesema imeingia mkataba na Savara kwa kuwa wanaamini atasaidia kuzinyanyua bidhaa za kampuni hiyo kuwafikia wateja wengi.