You are currently viewing SERENA BATA AKANUSHA MADAI YA KURUDIANA NA SIPAPA

SERENA BATA AKANUSHA MADAI YA KURUDIANA NA SIPAPA

Kwa muda sasa, kumekuwa na majabizano makali kati ya sosholaiti maarufu nchini Uganda Sipapa na mpenzi wake wa zamani Serena Bata. Sipapa amekuwa akimshutumu  vikali Serena Bata  kwa kutunga nyimbo zilizomlenga moja kwa moja.

Kwenye mahojiano yake wiki kadhaa zilizopita,  Sipapa alisikika akimuonya serena bata akome kumtaja kwenye nyimbo zake ambapo alienda mbali na kutishia kugoma kumpa msaada wa kifedha ambao anadai amekuwa akimpa.

Sasa katika mahojiano mapya, msanii Serena Bata ameibuka na kukanusha madai ya kurudiana na Sipapa, kwa kusema kwamba hawawezi fanya tena kazi na meneja wake huyo wa zamani.

Hitmaker huyo wa “Binuma” amedai kwamba sio kila wimbo anaoimba unamlenga sipapa kwani amekuwa akitoa muziki kwa ajili ya mashabiki zake.

Hata hivyo Serena Bata amesema juhudi za sipapa kumshawishi waanzisha mahusiano mpya ya kimapenzi hazitafanikiwa  kwani amemsahau kabisa kwenye maisha yake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke