Mshambuliaji wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Sergio Aguero ametangaza kustaafu soka kufuatia maradhi ya moyo.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na mwandishi Gerard Romero ambaye amejikita kwenye kutoa taarifa za Klabu ya Barcelona.
Maamuzi hayo tayari yameshafikiwa, klabu ya Barcelona imepewa taarifa huku ikipanga kutangaza rasmi wiki ijayo.
Gwiji huyo wa zamani wa Klabu ya Manchester City alipatwa na maradhi ya moyo (cardiac arrhythmia) kwenye mchezo dhidi ya Alaves ambao ulimalizika kwa Sare ya 1-1.