Mwanamke mmoja raia wa Kenya ambaye ni shabiki mkubwa wa mwanamuziki Willy Paul ameshindwa kuficha upendo wake kwa msanii huyo kiasi cha kuchora tattoo jina lake kifuani .
Shabiki huyo aliyetambuliwa kama Lizah Njeri awali alikuwa ameandika bango au poster akikiri mapenzi yake kwa mwanamuziki huyo ambapo alitembea katika mitaa ya Nairobi akiwa amebeba bango lililokuwa na jina na mawasiliano yake.
“Willy Pozee mwanaume wa ndoto yangu. Wewe ni crush wangu wa maisha, mimi ni Lizah Njeri naahidi kukupenda milele. ”
Kukiri mapenzi yake kwa willy paul kupitia maneno ya bango haikutosha, Alienda mbali Zaidi na kuchora tattoo kifuani mwake kwa wino wa kudumu kwa maneno yaliyosomeka ‘Pozee’.
Akizungumza katika mahojiano na Trudy Kitui, Lizah Njeri alisema anampenda sana Willy Paul na matamanio yake ni kwamba siku moja watakuwa marafiki wakubwa na kuishia kuwa wapenzi.
Lakini Pia alikiri kutumia picha ya willy paul kama wallpaper kwenye simu yake.