You are currently viewing SHAIRI KONGWE LILOANDIKWA NA RAPA TUPAC SHAKUR LAPIGWA MNADA KWA SHILLINGI MILLIONI 34

SHAIRI KONGWE LILOANDIKWA NA RAPA TUPAC SHAKUR LAPIGWA MNADA KWA SHILLINGI MILLIONI 34

Shairi kongwe ambalo liliandikwa na marehemu Tupac Shakur kipindi akiwa na umri wa miaka 11, kwa ajili ya kumpa zawadi Jamal Joseph na wanaharakati wa chama cha Black Panther, linapigwa mnada na kuuzwa kwa zaidi ya shilling million 34 za Kenya.

Chapisho hilo ambalo halikuwahi kuachiwa rasmi linauzwa ikiwa ni takribani miaka 40 baada ya rapa huyo kuliandika kama zawadi kwa Jamal Joseph ambaye alikuwa na umri wa miaka 16 kipindi hicho akiwa miongoni mwa wanaharakati 21 akiwemo pia mama yake mzazi Tupac, Afeni Shakur ambao walikamatwa kwa tuhuma za kupanga kulipua bomu kwenye vituo vya polisi mjini New York.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke