You are currently viewing SHAKIRA AKABILIWA NA KESI YA KUKWEPA KULIPA KODI UHISPANIA

SHAKIRA AKABILIWA NA KESI YA KUKWEPA KULIPA KODI UHISPANIA

Mwimbaji kutoka Colombia, Shakira anakabiliwa na kesi nchini Uhispania kwa madai ya ulaghai wa kulipa kodi, kulingana na vyombo vya habari nchini humo.

Waendesha mashtaka wa serikali wanadai Shakira alishindwa kulipa ushuru wa mapato ya kibinafsi na mali kati ya 2012-2014, ambayo kwa sasa ina thamani ya takriban dola milioni 15, madai ambayo ameyakanusha.

Shakira alitaja mashtaka yake kuwa “uongo” katika mahojiano na jarida la Elle mapema mwezi huu, akisema “Nililipa kila kitu walichosema ninadaiwa, hata kabla ya kufungua kesi. Kwa hivyo hadi leo, nina deni la sifuri kwao.”

Mamlaka za Uhispania zinadai nyota huyo aliishi nchini humo kwa muda wa siku 183 kila mwaka kati ya 2011 na 2014, lakini Shakira alikanusha madai hayo pia na kwa mujibu wa mawakili wake, makazi ya msingi ya staa huyo kwa wakati huo yalikuwa nchini Bahamas.

Katika hatua nyingine, Jaji wa mahakama moja huko Barcelona inayoshughulika na shauri hilo, ameamuru kesi hiyo isogezwe mbele, licha ya kutoweka wazi tarehe ya kuanza kusikilizwa tena.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke