You are currently viewing SHAKIRA AKIRI KUMPENDA GERARD PIQUE LICHA YA NDOA YAO KUVUNJIKA

SHAKIRA AKIRI KUMPENDA GERARD PIQUE LICHA YA NDOA YAO KUVUNJIKA

Mwanamuziki Shakira bado anaumizwa na kuvunjika kwa penzi lake na Gerard Pique, ameripotiwa kukasirika baada ya kuona video ambayo inamuonesha nyota huyo wa Barcelona akidendeka na mpenzi mpya, binti wa miaka 23 anayeitwa Clara Chia Marti.

Tovuti mbali mbali nchini Uhispania zinaripoti kwamba Shakira ameshikwa na gadhabu baada ya kumuona Pique ambaye waliachana mwezi June mwaka huu akionesha ushababi huo hadharani kinyume na makubaliano yao kwamba waheshimu faragha mbele ya watoto wao kwa angalau mwaka mmoja baada ya kuachana.

Wawili hao waliachana kwa sababu za usaliti ambapo Shakira alidaiwa kumfumania Pique akiwa na mwanamke mwingine. Mrembo Clara Chia Marti anadaiwa kuwa Afisa Mahusiano kwenye kampuni ya Pique na penzi lao lilianza miezi kadhaa nyuma

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke