Mwigizaji wa Bongo Movie Shamsa Ford amewataka vijana kujitenga na fikra za kizamani za kuwachukulia wapenzi wao wa zamani kama maadui huku akimtolea mfano ex wake rapa Nay wa Mitego.
Shamsa kupitia ukurasa wake wa Instagram amemwagia sifa Nay kuwa wa tofauti na wapenzi wake wengine kwa sababu hajawahi kumzungumzia vibaya tangu walipoachana na amemshukuru kwa hilo.
“Nakushukuru kwa kitu kimoja tu. Unaniongelea vizuri sana kwa watu tofauti na MAEX wengine. Tangu tumeachana sijawahi kusikia ukinizungumzia vibaya. Kupitia wewe vijana wanatakiwa kujua kuwa kuachana si VITA na wala hutakiwi kumuongelea vibaya mwenzio. COUSIN @naytrueboytz I SALUTE U” – ameandika.
Utakumbuka, Nay wa Mitego na Shamsa Ford waliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi miaka ya nyuma na baadae kuachana kabla Shamsa hajaolewa na mfanyabiashara Chid Mapenzi.