You are currently viewing SHATTA WALE AMCHANA REMA KWA MADAI YA KUDHALALISHA WANAWAKE WA GHANA

SHATTA WALE AMCHANA REMA KWA MADAI YA KUDHALALISHA WANAWAKE WA GHANA

Siku chache baada ya kuwatolea uvivu mashabiki na wasanii kutoka Nigeria, mwanamuziki mkali wa dancehall kutoka Ghana Shatta Wale ,amemchana mwanamuziki kutoka Nigeria Rema kwa kile alichodai kuwa ni udhalilishaji dhidi ya wanawake wa Ghana.

Hii ni baada ya Rema kupitia ukurasa wake wa Twitter kusema kwamba anataka wasichana 10 wa Ghana watulize akili yake kama njia ya kupunguza mawazo yake.

Sasa akijibu tweet ya mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 21 Shatta Wale amemkashifu Rema kwa kuwadharau na kuwavunjia heshima wanawake wa Ghana.⁠⁣

Hivi karibuni mwanamuziki huyo mkubwa nchini Ghana alichukua headlines katika mitandao ya kijamii akidai kuwa wasanii na mashabiki wa Nigeria ni wabinafsi ikija suala la kusapoti muziki wa mataifa mengine.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke