Mkali wa muziki wa dancehall kutoka Ghana Shatta Wale ameibuka kuwachana mashabiki wa muziki wa nigeria kwa kushindwa kutoa sapoti kwa muziki kutoka kwenye mataifa mengine.
Shatta ametumia ukurasa wake wa twitter kutweet mfululizo wa tweets zinazo kosoa na kushambulia tabia alizo ziita ubinafsi za wasanii na mashabiki wa Nigeria.
Lakini pia Shatta Wale ametolea mfano wa kile alichowahi kuzungumza mwanamuziki Mr Flavour akimtaja mwanamuziki aDiamond Platnumz kutoka Tanzania ni msanii mkubwa kwenye namba za mtandao wa YouTube kuliko wasanii wengi wa Nigeria lakini ni mara chache sana mashabiki nchini humo kumzungumzia ama kusapoti muziki wake.