You are currently viewing SHEEBAH ALAANI KITENDO CHA KUDHALALISHWA KINGONO KWENYE MOJA YA ONESHO LAKE

SHEEBAH ALAANI KITENDO CHA KUDHALALISHWA KINGONO KWENYE MOJA YA ONESHO LAKE

Aliyekuwa mwimbaji wa Team No Sleep Sheebah Karungi amemtolea uvivu mwanamume mmoja ambaye alimdhalilisha kijinsia akiwa jukwaani kwenye onyesho lake lilofanyika wikendi hii iliyopita.

Kupitia video aliyoshare kwenye instagram yake Sheebah Karungi amesimulia jinsi mwanamume huyo alimvunjia heshima mbele ya timu yake kabla ya kupanda jukwaani wakati wa onyesho lake na kisha kuanza kumshika shika bila idhii yake.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Pim Pim” amesema kitendo cha mwanamume huyo kumdhalilisha kilimkasirisha kiasi cha kutaka kususia shoo yake lakini ilibidi aheshimu kazi yake kwa kuendelea na onesho lake.

Sheebah amehoji ni kwa nini wanaume wamekuwa wakiwachukulia wanawake kama vyombo vya starehe kabla ya kuwashauri wawaheshimu wanawake kama wanavyotaka binti zao waheshimiwe.

Hata hivyo mashabiki wa sheebah wameonekana kukemea kitendo hicho, wakibainisha namna unyanyasaji wa kijinsia umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu huku Wengine wakimtaka amwanike hadharani mwanaume aliyemnyanyasa kijinsia.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke