Inaonekana Msanii nyota nchini Uganda Sheebah karungi anaendelea kujitenga na meneja wake wa zamani Jeff Kiwa.
Taarifa mpya ni kwamba mrembo huyo amefuta utambulisho wa lebo ya Team No Sleep kwenye bio yake kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.
Lakini pia amemuondoa Jeff Kiwa na mpenzi wake Mutoni Entana kwenye orodha ya watu anaowafuata kwenye mtandao wa instagram.
Jeff kiwa na Sheebah hawajathibitisha rasmi kama wamevunja uhusiano wao ila wamekuwa wakitupiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii.
Ikumbukwe kwa sasa sheebah anaendesha shughuli zake za kibiashara kupitia kampuni yake ya Sheebah business limited huku jeff kiwa akiwa anapromote msanii wake mpya Rahmah Pinky.