You are currently viewing SHEEBAH KARUNGI AMKANA HADHARANI CINDY SANYU

SHEEBAH KARUNGI AMKANA HADHARANI CINDY SANYU

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Sheebah Karungi amemkana hadharani msanii mwenzake Cindy Sanyu ambaye ni rais wa Muungano wa wanamuziki nchini humo.

Kupitia video aliyoishare kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram Sheebah amesikika akisema kuwa hamfahamu kabisa rais wa sasa wa muungano huo huku akimpigia upatu King Saha ambaye pia ametia nia ya kugombea wadhfa wa urais katika muungano wa wanamuziki nchini Uganda.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Nkwata Bulungi” amemwagia sifa King Saha akidai kwamba ndiye mkombozi wa tasnia ya muziki nchini Uganda ikizingatiwa kuwa ana ndoto ya kupigania suala la hakimiliki ambalo kwa muda mrefu limewaathiri wasanii wengi kwenye shughuli zao za kisanaa.

Hata hivyo amewataka mashabiki zake kuunga mkono azma ya King Saha kuwa rais wa muungano wa wasanii kwenye uchaguzi ambao utafanyika hivi karibuni.

Kwenye uchaguzi huo King Saha atachuana na Daddy Andrea pamoja na Cindy Sanyu ambaye kwa sasa ni rais wa Muungano wa wanamuziki nchini Uganda.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke