You are currently viewing Sheebah Karungi aweka wazi manyanyaso aliyoyapitia kwenye kundi la Obsession

Sheebah Karungi aweka wazi manyanyaso aliyoyapitia kwenye kundi la Obsession

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Sheebah Karungi amefunguka tusiyoyajua kuhusu uhusiano wake na wasanii wa kundi la Obsessiom ambalo lilimtoa kimuziki.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema wasanii wa kundi hilo walimbana kisanaa kiasi cha kumtenga kwenye baadhi ya shughuli zao za muziki.

Hitmaker huyo “Muwomya” amesema kutokana na changamoto alizopitia mikono mwa wasanii wa kundi la Obsession hakukataa tamaa kwenye ndoto yake ya kuwa mwanamuziki mkubwa nchini uganda na ndio maana akajitoa kwenye kundi hilo kuendeleza muziki wake kama msanii wa kujitegemea.

Utakumbuka Sheebah Karungi amekuwa kwenye muziki kwa takriban mwongo mmoja uliopita na watu walifahamu kwenye tasnia ya muziki Afrika Mashariki kupitia wimbo wake uitwao Ice  Cream.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke