You are currently viewing SHEEBAH WAVURUGANA NA MENEJA WAKE JEFF

SHEEBAH WAVURUGANA NA MENEJA WAKE JEFF

Taarifa  zinazotembea kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa zinadai kuwa mwanamuziki  Sheebah Karungi kutoka Uganda amejiondoa kwenye uongozi wake wa Team No Sleep ambao unasimamiwa na  Jeff  Kiwa

Sheebah Karungi, aliyekuwa mwanachama wa  kundi la The Obsessions, alijiunga na Team No Sleep mwaka wa 2013 na tangu wakati huo ametengeneza jina kupitia muziki wake barani Afrika.

Kwa miaka ambayo amekuwa kwenye muziki, ametoa ngoma kali, ameshinda tuzo nyingi,lakini pia amekuwa mfanyabiashara mkubwa ambaye anaangaliwa na vijana wengi nchini Uganda.

Tetesi mpya zinadai kuwa Sheebah  na meneja wake Jeff Kiwa wameingia kwenye ugomvi kutokana na masuala yanayohusiana na pesa.

Kulingana Mwanahabari maarufu nchini Uganda Jenkins Mukasa Team No Sleep inamtafuta msanii mpya atakayechukua nafasi ya Sheebah. Jenkins amesema kwa sasa Sheebah anasimamiwa na mtu aliyekuwa anaratibu shows zake akiwa chini ya Team No Sleep

Hata hivyo Sheebah hajatoa tamko rasmi kuhusu uvumi huo ikizingatiwa kuwa hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo kuripotiwa kuachana na Team No Sleep.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke