Msanii wa muziki na mjasiriamali nchini Tanzania Shilole amelizwa na tukio la mauaji ya mrembo maarufu wa shughuli za urembo (Make up artist) aliyeuawa kwa kupigwa risasi saba kichwani.
Kupitia waraka mrefu aliouandika kupitia ukurasa wake wa Instagram Shilole amesema kuwa ndoa siyo jela, na mtu akishindwa na masuala ya ndoa anapaswa kuondoka kwani ndoa za siku hizi siyo kama za zamani ambazo mtu anaweza vumilia.
Hitmaker huyo wa “Pindua Meza” amesema kuwa kama mwanaume hamjali mke wake na anampiga kila wakati ni vyema mwanamke achane nae kwani anaweza kumsababishia matatizo.
Mwanamke huyo aitwaye Swalha aliuawa kwa kupigwa na risasi na mumewe usiku wa kumkia Jumapili ya Mei 29 mwaka 2022. Tukio hilo limetokea nyumbani kwa wanandoa hao huko Buswelu nchini Tanzania huku chanzo kikielezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.