Mwanamuziki na mjasiriamali kutoka Tanzania Shilole amewachana baadhi ya wanaume wa mjini ambao wanapenda sana kujiremba kupita kiasi.
Katika mahojiano na Refresh ya Wasafi TV Shilole amewataka wanaumme wa sampuli hiyo kuacha hulka ya kuiga watoto wa kike kwa sababu wanajaribu kushindana na wanawake katika jamii.
Lakini pia mwanamama huyo ametoa changamoto kwa wanaume kujituma katika maisha badala ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja kwa ajili ya kujipatia kipato.
Hata hivyo haijabainika ni kitu gani kilimpelekea mwanamuziki huyo wa Bongofleva kuibua madai hayo ila walimwengu kwenye mitandao wanadai anatengeneza mazingira ya kuzungumziwa katika vyombo vya habari.