Mwimbaji nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria Simi, ameachia rasmi album yake mpya iitwayo “To Be Honest”.
Album hiyo ina jumla ya mikwaju 10 ya moto huku ikiwa na kolabo 3 kutoka kwa wakali kama Adekunle Gold, Fave na Deja.
To Be Honest ina nyimbo kama Story Story, No Joy, Balance, Born Again na tayari inapatikana kwenye mitandao yote ya ku-stream muziki duniani.
Hii inakuwa album ya tano kutoka kwa mtu mzima Simi baada ya “Restless II” iliyotoka mwaka 2020.
Album zake nyingine ni pamoja na “Chemistry” (2016), “Simisola” (2017) na “Omo Charlie Champagne” (2019).